Thursday, 14 September 2017

Nguvu ya maombi - Shuhuda



Karibuni kwenye wekeend ya kudeclare nguvu ya maombi. Tunajua kwa namna yoyote kuna hitaji ulilowahi kumwomba Mungu akakujibu. Hata kama ni kitu kidogo kiasi gani, Mungu anapenda shukrani.

Lengo la jambo hili ni kumrudishia Mungu sifa na utukufu kwa baraka anazotupa kila siku.

Pia kuwapa moyo waliokata tamaa. Unaweza kumsaidia mtu yoyote kwa ushuhuda wako. Kama watoto wa Mungu tunapaswa kusaidiana kwa hali yoyote, na moja wapo ya njia ya kusaidiana ni kupeana moyo.



Inawezekana bado una matatizo mengi makubwa ambayo hayajajibiwa, lakini inapaswa kushukuru kwa kila jambo, na hata yale tunayoyaona ni madogo.

Jambo hilo unaloliona ni dogo Mungu anatengeneza njia kupitia jambo hilo na utaona mafanikio ukiwa mwaminifu.



Njia za kututumia ushuhuda wako ni:


Facebook page yetu: Habari Njema Kwetu.

 Tutalinda privacy yako. Hatutaweka jina lako hadharani, au labda upende mwenyewe.

Karibuni sana. Mwisho wa kutoa shuhuda itakua Jumapili Tar 17 September.

Mungu awabariki.


No comments:

Post a Comment