Katika maisha haya unaweza kuishi kwa kutegemea vitu viwili:
1. Kumtegemea Mungu
2. Kutegemea akili zako mwenyewe ( Akili itakutuma kufanya chochote ikiwemo kutegemea nguvu za giza)
Lakini ukweli ni kwamba kila jambo ulilofanikiwa ni kutokana na neema ya Mungu. Kwa sababu sisi ni watoto wa Mungu. Mungu hana upendeleo katika kutoa baraka. Aliumba watu wote na ana upendo kwa watu wote sawa sawa.
Kwa hiyo usikate tamaa pale unapoomba, na unaona ambao hawaombi wala hawamjui Yesu wanafanikiwa. Baraka ni zile zile, na mtoaji ni yule yule. Endelea kuamini tu Mungu atamimina baraka zake. Usijaribu kukata tamaa, huwenda siku unayokata tamaa na kuacha kumtegemea Yesu ndio siku aliyopanga Baraka zake zionekane kwako.
Kuna tofauti kati ya wewe unayemjua Yesu na mwingine, wewe utapata baraka za kudumu, amani na furaha siku zote. Hata katika majaribu utapita kwa ushindi mkubwa na utaona njia ya kutokea haraka, kwa sababu ya nguvu iliyopo ndani yako.
Kila tunachoomba Bwana Yesu alishatoa miaka 2000 iliyopita, alipoutoa uhai wake kwa ajili yetu. Neema aliyoachilia kwetu ndiyo inayotupa kila kitu tunachohitaji.
Hatuombi ili mafanikio yaje, bali tunaomba ili mafanikio yaonekane kwetu. Tayari mafanikio yapo, ila ni sisi kuomba ili yaonekane kwetu.
Neema ya Mungu ndiyo inayotupatia kila tunachohitaji. Na unapata unachohitaji kwa imani. Unavyoamini ndivyo neema ya Mungu inamiminika kwako.
Usijaribu kumfanya Bwana Yesu arudi msalabani akupe mahitaji yako, tayari alishafanya hivyo. Unachotakiwa ni kuamini kile alichofanya, kisha omba neema iliyotokana na alichofanya ije kwako.
Dhambi:
Kwa sababu ya udhaifu wetu, mara nyingi tunamkosea Mungu. Ukishafanya dhambi inazuia baraka za Mungu kwako. Lakini Mungu ametoa msamaha wa dhambi kupitia Yesu Kristo. Unapofanya dhambi, unapaswa kukiri kwa Mungu kua unajua umekosa, na yeye atakusamehe.
Warumi 3:23-25.
Kupitia neema ya Yesu Kristo, tumehesabiwa haki. Na haki hii tumeipata kwa imani. Ni muhimu kuelewa cha kufanya unapofanya dhambi. Hakuna aliye mkamilifu. Ukishatubu dhambi zako Mungu atakusamehe na kuachilia baraka zake kwako.
Unaweza kuishi kwa kutegemea akili zako, ujuzi wako, usikumbuke kuomba na ukafanikiwa. Lakini kuna tofauti kubwa. Jaribu leo kumtegemea Mungu na kumshirikisha kila unachofanya, utaona tofauti ya mafanikio.
Jambo la muhimu zaidi, pamoja na mafanikio tunayopata kutokana na neema ya Mungu kwetu kwa kumtegemea, ni baada ya maisha haya. Tunaenda mbinguni kukaa nae na kufurahia maisha ya juu zaidi ya haya.
Kumtegemea Yesu hakuishii hapa duniani tu, bali tunauangalia msalaba unaotuongoza kueleka paradiso kwake. Kwa hiyo tunaenjoy maisha ya mafanikio ndani ya Yesu hapa duniani, wakati huo tukitazamia maisha bora na yenye furaha zaidi mbinguni.
Ubarikiwe.
No comments:
Post a Comment