Sunday, 2 July 2017

Faida za kumeditate kupitia Biblia


Habari Mpendwa, 
Karibu tutafakari neno pamoja. Hapa ninaeleza njia inayonisaidia mimi, ambayo nilijifunza na naendelea kujifunza kwenye Biblia  kila siku. Pengine mtu mwingine ana njia yake ya kukaaa kwenye uwepo wa Mungu na inamsaidia. 

Kujiweka uweponi mwa Mungu (presense of God)  kunaweza kutokea kwa njia nyingi. Mimi napenda zaidi kwa njia ya kutafakari neno lake (meditation), kwa sababu nna uhakika  na neno lake. (Mithali 30:5, Waebrania 4:12)
Meditation kwa kiswahili ni "kutafakari". Kila mmoja anaelewa maana ya kutafakari. Kutafakari (meditation) ni kitendo cha kutoa kipaumbele kwa kitu kimoja tu, au kuwaza na kusoma kitu kimoja kwa muda fulani ukiwa umetulia, kwa lengo la kujifunza, au kurelax. 


  Kuna mistari mingi ya Biblia imeeleza kutafakari neno la Mungu. Kuna aina nyingine za meditation, lakini mimi hapa ntazungumzia Christian Meditation.  Christian Meditation ni kutafakari neno la Mungu kwa mujibu wa Biblia takatifu, kwa muda fulani kwa kina ili mawazo yako yawe kama ya Yesu, 1 Cor 2:16. 
 Faida ya Kutafakari neno la Mungu (meditate)


1. Unakua na nia ya Yesu. (mind of Christ)
1 Cor 2:16. Ukiwa na nia ya Yesu unapata mambo yote mazuri kutoka kwake. Yohana 15:15, Yohana 16:13-16. Hakika utakua na hekima ya hali ya juu. 

2. Utazaa matunda mema
Yohana 15:4-5, Yohana 14:3-4. Ukikaa ndani ya Kristo unaijua njia ya kwenda kwake, popote alipo na wewe upo. Hata katika majaribu hutaogopa wala kuanguka. 

3. Una uhakika na njia ya kwenda mbunguni
Yesu alisema yeye ni njia kweli na uzima, mtu haendi kwa Baba ila kwa njia ya yeye.Yohana 14:6. Hutapotea kamwe ukikaa ndani ya Kristo. 

4. Hutashawishika na dhambi
Shetani kazi yake ni kudanganya (Deception). Ili usitekwe na mawazo yake uingie dhambini, meditate. Zaburi 4:4. Utaona mawazo yako saa zote ni safi huna wasiwasi wa kuanguka. Tunajua miili yetu ni dhaifu, lakini ukikaa ndani ya Kristo kila dakika, sio rahisi kuwaza mambo yasiyompendeza Mungu. Na hata tukianguka, neema ya Mungu ilivyo kuu, hutuinua tena, na Mungu hutusamehe dhambi zetu na kuzisahau, tunapata nguvu ya kuendelea. 

5. Upo salama (protection)
Ukimeditate na kukaa ndani ya neno la Mungu, upo salama. Huna wasiwasi wala woga. Kumb 31:8, Zaburi 18:2, Zaburi 32:7, 2 Thesalonike 3:2-4. Mistari ipo mingi sana ya ahadi ya Mungu kukulinda. 
Na faida zipo nyingi sana za kutafakari neno la Mungu. Kadri utakavyojizoesha na kuendelea ndio utakavyoona faida nyingi.
Jinsi ya Kumeditate
Kwanza kabisa kuna makala nyingi mitandaoni zinaelezea njia za kumeditate. Lakini mimi sikusoma hizo zote, nilianza tu kufanya kwa kadri nlivyoongozwa na Roho wa Mungu. 

1.  Omba Roho Mtakatifu akuongoze
Yohana 16:13. Roho wa Mungu atakufundisha mambo yote, na utaweza kuconcentrate vizuri bila vikwazo. Hili ndio jambo la msingi kuliko yote, kwa sababu kwa akili zetu wenyewe hatuwezi kamwe. Yohana 15:5. 

2. Chagua mistari ya Biblia unayotaka kusimamia
Kila mtu hupitia mambo mbalimbali katika maisha ya kila siku. Mara zote tunahitaji maneno ya kutia moyo ili tuweze kushinda kwenye kikwazo tunachipitia. Mimi hua nachagua mistari mitatu au mitano yenye ahadi ya Mungu kutokana na ninachopitia, kisha ninaikariri kichwani, hata kama sio neno kwa neno. 
Naiandika kwenye kanote book nachoweza kutembea nacho popote, au kwenye simu, kisha nakua nairudia siku nzima, popote nilipo. Hata kama nipo kwenye stress kubwa kiasi gani, nakua naisema kichwani. baada ya muda inakaa moyoni. Kwa kuongozwa na Roho, mistari ile haitoki moyoni mwangu. Najikuta naitafakari kwa kina sana, na hapo napata moyo wa kuendelea na kazi  huku nikisubiri ahadi ya Mungu kwenye hiyo mistari itimie. 

Mara nyingi zaidi hua napenda kutafakari kazi za Mungu. Hii inanijenga, hata kama sipo kwenye jaribu, nakua nautambua ukuu wa Mungu! Na mistari hiyo hunisaidia pale napopata kikwazo, nakumbuka Mungu alivyo mkuu.
 
Sio mara zote unapata matokeo uliyokua unawaza, lakini, Mungu ana mipango mizuri sana na sisi, no doubt. So matokeo siku zote ni mazuri sana, tena sana. Na unakua na amani ambayo ni ya ajabu, hujui kwanini una amani pamoja na mambo unayopitia!

Mifano miwili ya meditation
Hebu tuangalie mifano miwili ya meditation ambayo unaweza kufanya.

1. Ukipita katika jaribu.
Hapa unahitaji kupewa moyo na kufarijiwa ili uwe na amani na uweze kushinda. Chochote unachopitia, Biblia ina jibu. 
Labda unahitaji mistari hii: Mathayo 19:26, 1 Cor 10:13, Yakobo 1:2, Zaburi 3:3, Yeremia 29:11, Marko 11:23, Efeso 3:20, Warumi 8:37-39, Wafilipi 4:13. Mistari ipo mingi sana! Ukisoma Biblia unaiona.

2.Kumtukuza Mungu.
Sio vizuri kumkumbuka Mungu wakati wa matatizo tu, na wakati wa raha ukaendelea na shughuli zako. Wakati wote, popote tulipo ni wakati wa kumtukuza Mungu. Mungu bado ana mambo mengi sana ya kutupatia katika maisha yetu, hata kama unahisi tayari una kila kitu. 
Baadhi ya mistari ya kuutambua ukuu wa Mungu na kumsifu ni hii: 2 Samweli 22:50, Zaburi 9:1, Zaburi 149: 3, Danieli 2:23,  Yeremia 17:7, Warumi 5:5, Warumi 12:12, Zaburi 34:14. Hii nayo ipo mingi sana! Tusome Biblia.

Ukishika mistari kadhaa kwa kuongozwa na Roho mtakatifu, utaona unavyoishi kwa amani huku kila kitu kikienda sawa. 


Mungu atuongoze katika kuutafuta uso wake siku zote. Amen


No comments:

Post a Comment