Hello!
Ifike mahali ujielewe una thamani kiasi gani. Mara nyingi tunajikuta tunaonewa, tunafanya kazi zenye matatizo na changamoto nyingi, hata kama haikutakiwa kuwa hivyo. Kama hujajua thamani yako, kila unachofanya utafanya kwa shida. Kwa mfano, kama unasoma, either utafeli, au utafaulu kwa shida sana tena kwa kiwango cha chini. Ndoa yako kila siku ina shida hadi utaona ni kawaida kwa ndoa kua hivyo. Unatamani mke/mume hupati hadi unaona labda umepangiwa kukaa peke yako. Kazini kila siku ni changamoto, hakuna promotion wala kipato hakikui hadi utaona ni kawaida, maisha ni magumu. Kila eneo, either unafeli au unapita kwa shida sana.
Sasa, inawezekana hujaelewa thamani yako. Angalia point zifuatazo:
- Thamani yako inapatikana kwa Yesu Kristo pekee. Luka 15, angalia Yesu alivyoongea kwa mifano. Kondoo mmoja tu kati ya mia aliepotea akipatikana inakua sherehe. Hata kama una udhaifu na dhambi kiasi gani, jua kwamba Mungu anakupenda sana. Na ana mipango mizuri na wewe. Hata kama kuna watu wanakushusha chini, kukudharau, kukuambia huwezi, wewe elewa tu Mungu anakupenda na ana mipango mikubwa na wewe. Sema kwa sauti kila siku hata kama huna shida: “Mungu ananipenda. Na ana mipango mizuri na mikubwa kwa ajili yangu” . Itakusaidia sana pale unapokutana na jaribu.
- Mungu huwa hasemi uongo! Zaburi 89: 34. Soma biblia na shika ahadi zake uwe unamkumbusha kila wakati. Amesema hatalihallifu neno lake. Kama amesema it will be done, it will be done! Asije mtu yoyote kukuambia kinyume na alichosema Mungu. Kama Mungu amesema hakuna jaribu linalotujia lisilo la kawaida, na kwamba yeye ni mwaminifu hatatuacha tujaribiwe kupita tuwezavyo, basi amini hivyo. 1Cor 10:13. Hata kama unaona unashindwa na kila mtu anakwambia hivyo, wewe amini kile alichokisema Mungu, ndicho sahihi.
- Usiogope. Kuna watu wanapenda kuwajengea wengine hofu sana. Mtu anakufanya umuone yeye ni special sana kwa Mungu na huwezi kumfikia. Ukweli ni kwamba watu wote ni special kwa Mungu. Binadamu tunatekwa na mambo mengi ya dunia tunamsahau Mungu na kujikuta katika matatizo makubwa. Lakini pale tunaporudi na kumlilia, Mungu anatupokea tena kwa furaha sana. Malaika wanashangilia na Mungu anaanza kutekeleza mipango aliyokua amekuwekea. Kwahiyo usikubali shetani wala mtu yoyote akupe woga. Hatuna roho ya woga, 1 Timotheo 2:7, bali tuna roho ya Nguvu na ya Upendo na moyo wa kiasi. Hii nguvu tuitumie sana, kwa sababu tumepewa bure kabisa na inafanya kazi.
Napenda nikwambie, usiogope kufanya kitu kwa sababu watu watakuonaje. Fanya mambo yote sahihi, kwa kuanza kumshirikisha Mungu. Omba kwa bidii ili Mungu akuwekee hitaji (desire) inayotoka kwake. Kama unataka kuanzisha biashara, omba Mungu akupe kitu utakachopenda kufanya, ambacho kitampendeza yeye, hata kama hakimpendezi mtu mwingine, wewe unajua Mungu amekupa ufanye, lazima kitafanikiwa.
No comments:
Post a Comment