Ukipata majibu tofauti, kama hujaomba tafsiri kwa Mungu
unaweza kudhani hujajibiwa, na hapo unaweza kukata tamaa, au kumlalamikia Mungu
kwanini hajajibu. Unahitaji hekima na utiifu, na uaminifu ili Mungu aukuonyeshe
maana ya majibu hayo.
Leo tutazungumzia kile kipindi ambacho unasubiri. Je
unavumilia kiasi gani? Uvumilivu wako unakufikisha wapi, unakua unafanya nini
wakati wa kusubiri.
Tuangalie aina ya mambo ambayo wengi tunafanya wakati wa
kusubiri, baada ya kupata shida au haja fulani, wewe mwanamaombi ukapeleka haja
yako kwa Mungu unafanya nini kipindi hicho.
Mambo
ambayo wengi tunafanya wakati wa kusubiri majibu.
1. Wengi sana
hukata tamaa. Tunaacha kuomba, tunaendelea na maisha yetu, tunasema tunamwachia
Mungu. Hapo ni kama kumsusia Mungu, huombi lakini unasema unamwachia. Mara
nyingine unaweza ukaona majibu, lakini elewa kabisa sio kwa sababu ulimwachia
Mungu, ni kwa sababu Mungu wetu ni wa neema sana, akaona mtoto wake asipate
shida, akaamua kukupa haja yako.
2. Kulalamika.
Hapa unaweza ukawa unaomba lakini kwa kulalamika. Wakati mwingine kwa kulia
sana na kupiga kelele. Inawezekana Mungu akasikia na akajibu, lakini elewa
kabisa hajajibu kwa sababu umelalamika au kulia sana. Ni kwa sababu ya Neema
yake kwetu.
3. Matendo ya
mwili. Ukiwa unasubiri majibu, unakua mtoaji sana huku ukiamini kwa kufanya
hivyo ni kumfanya Mungu akupe majibu yako. Mara nyingine hata watumishi
wanasisitiza hilo, kwamba toa sadaka kiasi fulani, na utaona majibu yako.
Naomba uelewe kutoa ni jambo zuri sana na linalompendeza Mungu sana. Lakini
unatoa kwa malengo gani. Angalia usitoe kwa kumhonga Mungu, kumbuka yeye ndie
alitoa vyote tulivyo navyo. Ni mmilikia wa kila kitu, hakuna unachoweza kumpa
ili umfanye akusaidie.
Kwa hiyo, tunatoa ili kumwonyesha Mungu kuwa
tunamwamini kwa vyote tulivyo navyo, tunaamini yeye ndiye Mungu, ndiye mfalme
wamaisha yetu. Hatutoi ili afanye jambo fulani, hiyo ni wrong motive. Usiende mbele
zake huku ukimkumbusha ulitoa sadaka kwa
ajili ya majibu ya maombi yako.
Ni vyema tujue namna ya kukaa uweponi kwa Mungu wakati
wa kusubiri majibu ya maombi yetu. Tunaweza kuwa tunapitia mateso wakati wa
kusubiri, hayo yanakujenga ili uweze kuvumilia zaidi, usitetereke uwe na uwezo
wa kukabiliana na jambo lolote.
Somo la pili la uvumilivu litaendelea. Tujue jinsi ya kuweza kuvumilia, tunatakiwa kufanya nin wakati wa kusubiri, na
mengine mengi.
Ubarikiwe sana.

No comments:
Post a Comment