Habari wapendwa.
Nchi na vyote viijazavyo ni mali ya Bwana. Zaburi 24:11 pamoja na wote wakaao ndani yake. Tukumbuke tunapotafuta mwenye mali ni Mungu, ndiye aliyetuweka hapa na hata akatupa nguvu ya kutafuta.
Ili upate ni lazima umwangalie na umwombe yeye mtoaji. Usitumie njia nyingine yoyote kama kwenda kwa binadamu mwenzako (mganga) kuomba, kwa namna yoyote hutafanikiwa. Na mafanikio ukiyapata yatakupa stress na si ya kudumu.
Wazazi ni mfano mzuri wa jinsi Mungu anavyofanya kazi. Mwanao anapohitaji anakuja kwako, anakwambia shida yake. Ndiyo njia rahisi ya yeye kupata hitaji lake.
Ndivyo na sisi inapaswa tumwendee Mungu kumwambia mahitaji yetu. Unataka kupiga hatua kwenye biashara yako, kazi au chochote unachofanya, nenda kwake mwambie kwa unyenyekevu. Na yeye atakufanyia kama alivyoahidi.
Vitu muhimu vya kukumbuka katika safari yako ya kutafuta
1. Mungu ndiye mmiliki wa kila kitu na ndiye mtoaji.
Ujuzi na juhudi zako ni muhimu sana katika kufikia malengo yako. Ujuzi kwa njia ya kusoma shuleni, kujifunza kwa wengine, kusoma vitabu nk, na juhudi ya kazi inaweza kukuletea mafanikio. Lakini kumbuka kwamba, mafanikio hayo Mungu ndiye anaetoa. Ili uelewe vizuri, weka jambo hili kichwani na moyoni kwanza. Yaani, kitu cha kwanza unapoamka asubuhi kuingia kwenye shughuli zako, umwambie Mungu, naanza kazi zangu, lakini nakukabidhi kwanza wewe, uniongoze na kunifundisha na unipe riziki wewe.
Riziki inayotoka kwa Mungu inadumu. Na mafanikio yote yanayotokana na maombi yako kwa Mungu yanakua na baraka idumuyo. Baraka hiyo huongezeka kila siku na kubariki hata wengine. Ni muhimu tujue kumuweka Mungu kwanza kwa kila tunalofanya.
2. Ukimwambia Mungu unachohitaji atakujibu
Kuna watu wanaweza kubisha hili. Wengine wanabaki kumlaumu Mungu kwa sababu walichoomba hakijajibiwa, na kukata tamaa na kuamua kutegemea akili zao wenyewe.
Lakini kuna watu wengi sana wanaweza kukushuhudia maombi yao yalivyojibiwa. Na pia kuna ushuhuda mwingi sana unaozunguka maisha yetu. Hata ulivyo leo ni Mungu amekuweka hapo ulipo. Kwahiyo amini kua Mungu anajibu ukimwomba. Anaweza asijibu ulivyotaka wewe, lakini kwa kua anatujua kabla hatujazaliwa ana mawazo mema juu yetu, hicho alichokunyima ni faida yako. Tunapaswa kumshukuru hata mambo yakienda tusivyotaka. 1 Wafalme 2:3 wakati mfalme Daudi akikaribia kufa, alimwusia mwanae Sulemani. Jambo la kwanza alilomwambia ni kushika amri za Mungu. Kuwa mwadilifu mbele za Mungu. Kwa neema yake tunajua mema na mabaya. Kama unaona jambo unalotaka kufanya ili ujiingizie kipato ni wizi au utapeli, acha. Mungu ni mkuu sana, leta shauri lako umwombe akupe njia sahihi.
Njia pekee ya kupokea jibu lako ni kuwa na imani na uwezo wa Mungu. Amini anaweza, kabla ya yote.
3. Kuwa baraka kwa wengine.
Usiwe mchoyo! Mungu anakubariki ili na wewe uwe baraka kwa wengine. 2 Kor 9:8-11, Warumi 12:13. Kadri unavyotoa utazidishiwa. Hii ni formula inayoapply sehemu nyingi sana, hata wasio wakristo wanajua. Ukitoa unazidishiwa. Unapobarikiwa, angalia jamii inayokuzunguka na uwe baraka kwao.
Unapotoa sio kwamba unamwonyesha Mungu unatoa ili akuongezee, bali unamwonyesha Mungu kuwa unamwamini kwa kile alichokubariki nacho. Unamwamini Mungu kwa mali zako.
4. Mwisho kabisa, fanya kazi kwa bidii.
Mungu amekuweka hapo ulipo iwe ni biashara, kazi au chochote unachofanya kwa makusudi. Hata kama ni kidogo kiasi gani, fanya kwa moyo wako wote. Mungu haangalii elimu, au jamii uliyokulia, akitaka uwe tofauti na ukue hapo ulipo unakua. Kwa hicho kidogo ulichonacho kuwa mwaminifu na fanya kwa bidii zote. Mithali 12:11, Zaburi 90: 17. Kumbuka kumshirikisha Mungu katika kila hatua. Yeye ndie awe base ya biashara au kazi yako.
Muhimu: Mwamini Mungu kwanza, na hayo mengine utazidishiwa.
No comments:
Post a Comment