Tuesday, 4 July 2017

Unajua kusimama kwenye nafasi yako?

Esta Alipopata ujumbe kua watu wa kabila lake watauawa aliingia kwenye maombi  na wajakazi wake. Akatuma ujumbe kwa wayahudi wote wafunge pia. Kisha angeingia kwa mfalme bila ruhusa ili kujaribu kuwaokoa.

Akajisemea, "nami nikiangamia na niangamie" (Esta 4:16).

Esta alijiamini, kwa sababu alijua Mungu wake alivyo mkuu, mwenye ahadi za kweli na upendo wa ajabu.
Mungu alisikia maombi yake na  akawaokoa wayahudi. Mbaya wao Hamani alietaka kuwaangamiza akauawa.

Wewe kama mwanamke wa kisasa, pamoja kua smart kimavazi, nywele na fashion kwa ujumla, lakini simama kwenye nafasi yako pale unapoona mambo hayaendi vizuri. Kuwa muombaji, hatupaswi kuishi kwa mazoea au trend.

Funga kwa maombi, omba kwa ajili ya mume, watoto, wazazi, kazi, masomo, biashara nk.


Inawezekana kama Esta alivyokua, wewe ndie unaeweza kumsaidia mtu au kitu fulani kifanikiwe.
Labda mumeo amekwama, inawezekana maombi yako ndio yatakayoweza kumtoa. Na inawezekana wewe peke yako katika familia yake yote ndie mwenye nafasi ya kumuombea.
Haimaanishi wengine wakiomba hawatajibiwa, hapana. Lakini kuna mambo mengi sana yanayoendelea kwenye maisha ya watu. Kwahiyo chukua nafasi yako na umwambie Mungu, na yeye atajibu bila wasiwasi.

Yesu ametupa uhuru kabisa, ukiomba neno lolote kwa jina lake atasikia na atafanya. Bora uombe hata ikiwa muda mrefu kiasi gani lakini unajua ipo siku Mungu atajibu. Kuliko kuacha kuomba, unakosa matumaini, unaanza kuwa na mawazo mabaya na kukosa mwelekeo, unatafuta solution mbaya zenye hasara au changamoto nyingi.

Omba huku ukishukuru kwa kua Mungu ni mwaminifu anakusikia. Ameshajua tatizo lako kabla hujamwomba, ila anataka tu umwamini ili afanye makubwa maishani mwako..

Mwisho kabisa amini kua Mungu anasikia, na yeye ana nguvu na mamlaka, ana uwezo usioelezeka. Wakati unafanya kazi, biashara au kusoma kwa bidii, wakati huo huo endelea kuomba ili Mungu akuinue na kukupa mafanikio.

No comments:

Post a Comment