Mara nyingi huwa tunawaza vitu tusivyovitaka badala ya vile tunavyovitaka maishani. Watu huwa wanareact pale tu vitu wasivyotaka vinapotokea. Mfano tunapopata changamoto nyumbani, kazini, kwenye biashara au masomo, tunaanza kuwaza kufukuzwa kazi, kuachwa, kupata hasara, yani mambo yale tusiyotaka yatokee.
Sio vibaya kutumia rasilimali zako kuzuia changamoto, lakini kua makini usije ukawa unatumia maisha yako yote kufanya hivo. Kipato hakiongezeki wala hakuna maendelea yanayoonekana kwa sababu hujawekeza mawazo kwenye kuibua idea mpya za kujiendeleza.
Jinsi unavyoweza kuwekeza kwenye kila unachotaka, kwanza kabisa mpe Bwana Yesu nafasi kwenye kile unachofanya. Yoh 15:5--Mimi ni mzabibu; ninyi ni matawi, akaaye ndani yangu nami ndani yake, huyo huzaa sana; maana pasipo mimi ninyi hamwezi kufanya neno lolote.
Wagalatia 6:3—Maana mtu akijiona kua ni kitu, naye si kitu, ajidanganya nafsi yake.
Wekeza mawazo yako kwa Bwana Yesu na uombe mwongozo wake, ili hata changamoto zisiwe nyingi, na uweze kuzishinda. Tunajua kila kitu kina changamoto, lakini Yesu akisimamia, unasolve na kuendelea mbele.
Kwa uwezo wa Yesu pia utaweza kupata idea mpya za jinsi unavyoweza kuboresha unachofanya. Akili yako itakua mpya kila siku na utaweza kufocus.
Kwa uwezo wa Yesu pia utaweza kupata idea mpya za jinsi unavyoweza kuboresha unachofanya. Akili yako itakua mpya kila siku na utaweza kufocus.
Kama unafanya biashara badala ya kumaintain mtaji angalia unavyoweza kuukuza, usiogope kujaribu, angalia unavyoweza kufikia watu wengi zaidi, boresha bidhaa au huduma ongeza eneo unalofanyia biashara nk.
Kazini, badala ya kuepuka tu bosi asikugombeze, au kutumia system ile ile uliyoikuta, thubutu kujaribu. Angalia unavyoweza kuongeza ubora wa reports, kuzingatia muda, kutimiza deadlines, kupata promotion, kujiendeleza kimasomo nk.
Shuleni badala ya kusoma siku moja kabla ya mtihani, concentrate darasani, soma hata kama hakuna mitihani, tumia muda vizuri nk.
Ukifanya hivi unawekeza ‘long term’. Unaweza usione mafanikio hapo hapo, lakini baada ya muda utaona matunda ya kazi yako. Utakua umetumia mawazo, nguvu na muda wako kuwekeza kwa ajili ya baadaye.

Hii inawezekana hata kwenye mahusiano. Kama hujaoa/olewa na unataka iwe hivyo, badala ya kusubiri uone mtu ndio uanze kubadilika, badilika kuanzia sasa. Wekeza kwenye tabia yako, mwombe Mungu akufanye mke/mume bora kwa mwenzako kabla hata hajaja. Hii itakurahisishia kuishi kama wewe, badala ya kupretend ili kumridhisha mwenzako. Hutaweza kufanya hivyo kwa muda mrefu.
Epuka kuweka mawazo kwenye woga, wasiwasi, kujishtukia, kuogopa wengine wanakuonaje, hasira, na mambo mengine mabaya. Haya ni ya adui, hayatoki kwa Mungu. Adui akifanikiwa kukupa kimojawapo focus yako yote itakua jinsi ya kuzuia, na hutakua na muda wa kuwaza kuendeleza unachofanya.
2 Timotheo 1:7--Maana Mungu hakutupa roho ya woga, bali ya nguvu na ya upendo na ya moyo wa kiasi.
2 Timotheo 1:7--Maana Mungu hakutupa roho ya woga, bali ya nguvu na ya upendo na ya moyo wa kiasi.
Woga na wasiwasi wa kufeli kwenye jambo utakuja, ndio moja wapo ya njia ya shetani. Lakini wewe kwenye woga weka imani. Amini hayo ni mapito tu, na Mungu ambaye hajawahi kukuacha atakupitisha na hilo. Amini pia Mungu anakupenda sana, na hatakuacha uangamie kwa sababu alishakuokoa kupitia Yesu Kristo.
Kuwekeza mawazo na nguvu kwenye kile unachotaka na unachopenda kufanya kunaleta faida badae. Inakufanya ukue na uwe strong kwenye ushindani. Focus yako kwanza iwe kwa Mungu, wekeza mawazo yako kwake ili ayaongoze kwenye kuleta mafanikio ya kile unachofanya.

No comments:
Post a Comment