Mara nyingi hua tunapoteza muda mwingi sana kuwaza matatizo. Mtu mmoja unaweza ukashambuliwa na mambo mengi hadi ukakata tamaa ya maisha. Matatizo yapo mengi, na ni jukumu letu kutafuta njia ya kuyatatua.
Tunachokosea ni pale tunapojaribu kusolve kitu kimoja kimoja kwa kutumia akili zetu wenyewe. Sina maana usijaribu kutafuta suluhisho la matatizo yako, lakini je unaweza? Baadhi ya watu wanapata mawazo kwa sababu ya vitu vidogo sana na anajikuta anaharibu mambo mengine kwa sababu hiyo.
Tuangalie mstari huu, Waefeso 4:6 “Msijisumbue kwa neno lo lote; bali katika kila neno kwa kusali na kuomba, pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane na Mungu.”
Unadhani Mungu hatambui mambo unayopitia? Anajua kabisa, na pengine anasikitika unavyotumia njia tofauti kusolve tatizo lako. Ndio maana tunakumbushwa kuwa tusijisumbue kwa jambo lolote. Hapa hamaanishi utulie bila kujua suluhisho la shida yako. Ametoa njia mbadala ya kujisumbua, ni kusali, kuomba na kushukuru, haja zetu zijulikane na Mungu.
Mungu akishaona umempelekea haja yako atakupa mwongozo wa kutatua. Mstari wa 7 “Na amani ya Mungu, ipitayo akili zote, itawahifadhi mioyo yenu na nia zenu katika Kristo Yesu”
Mungu akishajua haja yako atakupa amani yake ipitayo akili zote ikuhifadhi moyo wako na nia yako. Hutakosa amani tena na kuwaza kupitiliza kwa sababu tayari una amani ya Mungu na atakuonyesha njia ya kumaliza shida yako.
Kuna msemo unaosema 'pray until something changes’ yaani omba hadi uone madadiliko. Usikubali adui akujazie matatizo kichwani uone umebeba mzigo ambao hakuna anaeweza kubeba. Hiyo ni trick ya kukufanya uone Mungu hakusaidii. Mungu anataka useme nae tu na uamini kua atafanya, nae atafanya.
No comments:
Post a Comment